28 Mei 2019 - 09:31
Mahmoud Abbas: Muamala wa Karne kamwe hautotekelezwa

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amejibu njama za Marekani, Israel na vibaraka wao wa Kiarabu za kupanga kuitisha mkutano wa "Muamala wa Karne" nchini Bahrain na kusema kuwa, mpango huo kamwe hautotekelezwa kwani njia ya kisiasa ndio utatuzi pekee wa kadhia ya Palestina.

(ABNA24.com) Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amejibu njama za Marekani, Israel na vibaraka wao wa Kiarabu za kupanga kuitisha mkutano wa "Muamala wa Karne" nchini Bahrain na kusema kuwa, mpango huo kamwe hautotekelezwa kwani njia ya kisiasa ndio utatuzi pekee wa kadhia ya Palestina.

Televisheni ya al Mayadeen imemnukuu Mahmoud Abbas akisema hayo usiku wa kuamkia leo Jumanne na kuongeza kuwa, mgogoro wa Palesitna unaweza kutatuliwa tu kwa njia za kisiasa na si kupitia vikao vya kiuchumi vyenye lengo la kuisahaulisha kabisa kadhia ya Palestina.

Ameongeza kuwa, muamala wa karne au muamala muovu utavurumishwa katika moto wa jahannam kama ambavyo pia kikao cha kiuchumi cha Bahrain kilichopangwa kufanyika mwezi ujao, nacho kitatumbukia katika moto wa jahannam.

"Muamala wa Karne" ni mpango wa Marekani ambao lengo lake ni kuangamiza haki za wananchi wa Palestina. Mpango huo umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa mpango huo, mji mtakatifu wa Quds watapewa Wazayuni, wakimbizi wa Palestina hawatokuwa na haki ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Wapalestina watamiliki tu vipande vidogo vya ardh vitakavyobakia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza.



/129